Quantcast
Channel: UTAMBUZI NA KUJITAMBUA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 54

Mwanamke: Ni jukumu lako kujipa muonekano wa kumvutia mumeo baada ya kujifungua

$
0
0
[​IMG]

Kwa mwanamke ni jambo la faraja kupata mtoto baada ya kuolewa, lakini kupata mtoto kunaambatana na mabadiliko ya mwili kwa mwanamke. Ni wanawake wachache sana wanaobaki na miili yao mara baada ya kujifungua, lakini wengi wao hupoteza muonekano wa awali na kuongezeka mwili au tumbo na hivyo kupoteza muonekanao wake wa awali.

[​IMG]
Mwanamke akifanya mazoezi

Jambo hilo kwa baadhi ya wanaume ambao mapenzi kwa wenzi wao ni muonekanao wa nje wa mwanamke jambo hilo huzua kero na kupoteza hamu ya kukutana kimwili na mwenzi wake kama awali. hapo ndipo tatizo la kuchepuka linapoanza.
[​IMG]
Mwanamke akifanya mazoezi ya kukimbia

Ingawa pia tatizo la baadhi ya wanawake kuhamisha mapenzi kwa watoto wao badala ya baba zao linasumbua ndoa nyingi, lakini hili la kupoteza muonekano na kuwa tipwatipwa limeonekana kuchangia wanaume wengi kupunguza mapenzi kwa wenzi wao.

Kwa ushauri tu, ni kwamba, wanawake wanapaswa kubadilika na kuanza kufanya mazoezi na kuzingatia mlo wao wa siku kwa kuacha kula hovyo hovyo ili kuepuka kupoteza muonekano wao wa awali. Si lazima kwenda kwenye nyumba za mazoezi kwa sababu kunahitaji gharama ambazo wengine si rahisi kuzimudu, lakini kwa mazoezi ya kutembea kwa umbali wa maili mbili kwa simu asubuhi au jioni kila siku na kufanya mazoezi ya kucheza mziki (Aerobics) kunaweza kusaidia kuweka mwili katika muonekano mzuri.


Ni ushauri tu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 54

Trending Articles